iqna

IQNA

IQNA-Kamanda mwandamizi wa Sarayal-Quds, tawi la kijeshi la Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina ametangaza kuwa, askari wapatao 40 wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameuawa au kujeruhiwa katika operesheni ya kijeshi iliyoratibiwa na wapiganaji wa Muqawama mashariki ya Ghaza.
Habari ID: 3480898    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/05

IQNA – Kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ameelezea kwa uchungu hali ya mateso ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akisema ni jambo linalomuumiza sana kila anapofikiria yanayoendelea katika eneo hilo.
Habari ID: 3480823    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/11

IQNA-Katika hali ambayo, meli ya "Madleen" iliyokuwa imebeba misaada ya kibinadamu ilikuwa imekaribia Gaza, majeshi ya utawala haramu Israel yalishambulia meli hiyo katika hatua iliyotajwa kimataifa kuwa ni uharamia, na kuwateka nyara abiria wake na hivyo kuzuia misaada hiyo kufika Gaza.
Habari ID: 3480818    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10

IQNA-Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa Linalowahudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amezitaka nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi kutenga tone tu la fedha zilizotajwa katika ‘makubaliano makubwa’ kati yao na Rais wa Marekani, Donald Trump, ili kusaidia wakimbizi wa Kipalestina wanaopambana kuendelea kuishi katika ardhi zao ambazo Israel imezikalia kwa mabavu na pia wale wanaoishi katika nchi jirani.
Habari ID: 3480762    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/30

IQNA-Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, katika mkutano na maafisa wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani, Vatican huko mjini Rome, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka za kimataifa kukomesha uhalifu unaoendelea kutendwa na utawala katili wa Israel huku Gaza, na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inafika katika eneo hilo lililozingirwa.
Habari ID: 3480732    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/24

IQNA-Shirika la Kimataifa la Uhamaji (IOM) limeripoti kwamba zaidi ya Wapalestina 97,000 wamehamishwa Gaza katika kipindi cha siku nne pekee, huku mashambulizi ya Israeli yakizidi kuwa makali katika eneo hilo lenye mateso.
Habari ID: 3480710    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/20

IQNA – Nchi wanachama wa Muungano wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (PUIC) zimetoa wito wa kuwekwa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Israel, huku utawala huo ukiwa unaendelea na vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza.
Habari ID: 3480695    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/17

Spika wa Bunge la Iran katika Swala ya Ijumaa Indonesia
IQNA-Spika wa Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge la Iran), Mohammad Baqer Qalibaf, ametoa wito kwa Waislamu kuimarisha umoja na kuwa sauti ya watu wa Palestina walioko Ukanda wa Gaza, ambao wanakumbwa na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Israel.
Habari ID: 3480692    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/16

Jinai za Israel
IQNA-Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Ghaza ametangaza leo Ijumaa kwamba ukanda huo ndilo eneo la mauaji ya umati ya kutisha zaidi katika siku za hivi karibuni kiasi kwamba Wapalestina 250 wameuliwa shahidi na Israel katika kipindi cha saa 36 zilizopita pekee.
Habari ID: 3480690    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/16

IQNA – Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kuwepo harakati za jamii ya kimataifa ili kusitisha mauaji makubwa ya kimbari ya karne hii. 
Habari ID: 3480607    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/28

IQNA – Kupitia taarifa kali kwenye mitandao ya kijamii, Mufti Mkuu wa Oman, Sheikh Ahmad bin Hamad Al-Khalili, amewakosoa vikali viongozi wa Kiarabu wanaoripotiwa kutoa wito wa kuwapokonya silaha wanamuqawama au wapigania ukombozi wa Palestina huko Gaza.
Habari ID: 3480550    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/16

IQNA – Indonesia iko tayari kutoa hifadhi ya muda kwa watoto na Wapalestina waliojeruhiwa kutokana na vita vinavyoendelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, amesema Rais Prabowo Subianto.
Habari ID: 3480518    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/09

IQNA-Kamati ya Ijtihad na Fatwa ya taasisi moja ya kimataifa ya wanazuoni Kiislamu imesisitiza kuwa kuanzisha Jihad dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Isarel unaoendeleza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza ni wajibu wa Kiislamu.
Habari ID: 3480496    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/05

IQNA-Mkuu wa Shirika la UN la Wakimbizi wa Palestina (UNRWA) ametahadharisha kwamba hatua ya utawala wa Israel kuweka mzingiro na kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza inapelekea eneo hilo la pwani kukaribia baakubwa la njaa.
Habari ID: 3480426    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/24

IQNA-Jamii ya kimataifa imebainisha hasira yake baada ya utawala katili wa Israel kuendelea na mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza, huku ikivunja makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyokuwa na lengo la kumaliza mzozo wake wa miezi 17 na Hamas.
Habari ID: 3480404    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/19

Matukio ya Palestina
IQNA-Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema upayukaji na vitisho vya Trump vinavuruga makubaliano ya kusitisha mapigano kwani vinauchochea utawala wa Kizayuni wa Israel kutotekeleza wajibu wake.
Habari ID: 3480318    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/03/06

Jinai za Israel
IQNA – Jumla ya wanawake na watoto 90 wa Kipalestina waliachiliwa kutoka magereza ya kuogofya ya Israel mapema Jumatatu kama sehemu ya kubadilishana wafungwa iliyohusishwa na makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na utawala haramu wa Israel.
Habari ID: 3480083    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/20

Gaza
IQNA-Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amepongeza makubaliano ya kustisha vita katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza kuwa nafasi ya Gaza katika kujitolea itasajiliwa katika historia.
Habari ID: 3480075    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/18

Jinai za Israel
IQNA-Idara ya Ulinzi wa Raia ya Gaza imetangaza leo Ijumaa kuwa Wapalestina wasiopungua 101, wakiwemo watoto 27 na wanawake 31, wameuawa shahidi katika mashambulizi ya Israel tangu kutangazwa makubaliano ya kusitisha mapigano juzi Jumatano.
Habari ID: 3480064    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/17

Muqawama
IQNA- Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina (Hamas) imeidhinisha pendekezo la kusimamisha mapigano kwa Ukanda wa Gaza ambayo yamefikiwa kwa upatanishi wa Misri na Qatar.
Habari ID: 3480060    Tarehe ya kuchapishwa : 2025/01/15